Wakazi wa Iringa wameifunga awamu ya kwanza ya Kilimanjaro Music Tour kwa kufurika katika uwanja wa Samora kushuhudia wakali wa muziki nchini wakitoa burudani bila kujali hali ya hewa ya baridi. Wakali kama Snura, Linex, AY, Mwana FA, Profesa Jay, Izzo Bizness, Joh Makini, Juma Nature, Mwasiti, Nikki wa Pili na Gnako Warawara walilishambulia jukwaa kwa masaa sita mfululizo na kuwakonga nyoyo maelfu waliojitokeza uwanja wa Samora kuwashuhudia. Ziara hiyo iliyozunguka mikoa mitano inatarajiwa kuendelea mwezi Agosti ikiwa ni kuupisha mwezi ramadhani na inatarajiwa kwenda mikoa ya Mbeya, Kigoma, Mtwara, Dodoma na kukamilishiwa Dar es Salaam.
Snura ndiye aliifungua Kili Music Tour kwa kuonyesha umahiri wake wa kulishambulia jukwaaTazama picha zaidi hapa