Ni mara nyingi Diamond Platnumz huwa anasema kuwa ana nyimbo nyingi sana alizoisha rekodi na bado anaendelea kurekodi kila kukicha, lakini sio nyimbo zote alizonazo zitapata nafasi ya kutoka kama official singles.
Kupitia Instagram yake hit maker wa ‘Number 1’ ameamua kuwaonjesha kidogo mashabiki wake wimbo mmoja ulioko kwenye maktaba yake.
“wakati Mwingine natamanigi hata mngepata dakika moja tu ya kuskia nyimbo nilizo nazo ndani, … hii inaitwa #Nitampata_wapi? sjui kina @babutale wataitoa lini… maana haipo kabisa katika list ya nyimbo zitolewazo… ila, kwakuwa nyie ni watu wangu wa nguvu nimeamua kuwaibia kidoogo, sjui watanimind!#GermanyWeekEnd.” – Diamond
“Kwa heshima yenu tu, hichi kipande cha mwisho… ( Alonifanya silali, jua kali, nimtafutie tukale, lakini wala hakujali… darling, akatekwa na wale….) #NITAMPATA_WAPI? #One_Of_Unreleased_Love_Song #GermanyWeekEnd”
Weekend hii Diamond na vijana wake wa Wasafi wako Ujerumani ambapo wamefanya show ya kwanza usiku wa jana.
30 Agosti 2014
Home
Diamond Platnumz
Music
Audio: Diamond aonjesha kipande cha wimbo wake ambao haujatoka ‘Nitampata wapi’
Audio: Diamond aonjesha kipande cha wimbo wake ambao haujatoka ‘Nitampata wapi’
Tags
# Diamond Platnumz
# Music
About New Jobs Tanzania
Music
Category:
Diamond Platnumz,
Music