Nikaona isiwe shida ngoja nikamuone roho yake itulie nipo njiani wazo likanijia…Nikapitia duka moja maarufu Sinza na kumnunulia zawadi ya viatu kama suprize nimejikoki mwenyewe naenda kwa babybaby…mademu bwana..!
Kufika akanipokea kwa bashasha na mabusu motomoto dady’s home..Yeye.. najua umechoka baby wangu kaa kwa kochi upumzike nataka nikutengenezee juice fresh unayo ipendaga..nikamwambia ngoja kwanza nikupe zawadi yako nikatoa vile viatu na kumpatia akafurahi sana na kuvijaribisha..vilimtosha na kumpendeza..Nikapewa busu lingine la sekunde kazaa.,
Akatoka kwenda kuandaa juice..huku simu yake na vile viatu akiwa ameviacha jirani na kochi nililokaa..Nikamuuliza simu yako inabando..akanijibu ndio..Nikaichukua nakuingia sehemu ya kubrowse internent ..akili ikanituma nifanye udukuzi kidogo nikafungua application yake ya watsupp mbona nilichoka..
Nilikuta msururu wa wanaume anaochati nao nakuwatumiana picha akiwa amevaa pichu tu nakukaa kimitego…huku wakiambiana ni jinsi gani wamemisiana kupeana utamu..kijasho kikanitoka. .nikajikaza mwenyewe na kuendelea kuperuzi kwa wote idadi ikafikia wanaume kumi na moja na kwa mtiririko wa chating yao wote waonekana wameshapewa utamu..Napenda kusema kitu kimoja hapa tangu nimeanza mahusioano nae tumefikisha mwaka sasa sikuwahi hata siku moja kuishika simu yake.,
Nilishikwa na hasira sana yani huduma zote ninazo mpatia kumbe nahudumia kahaba..nikamwita na kumuuliza aniambie hao watu ni akina nani..utetezi alionipa anasema ni marafiki zake nisimfikirie vibaya..
Nilitamani nimkate kofi moja la nguvu yani ushahidi wote ninao hapa unanijibu rejareja hivyo..nikamuuliza huo urafiki pamoja nakugongana..!we kweli kiboko sasa unataka nikupe cheo gani huu ni umalaya au kipaji...Akaanza kulia huku akiomba nimsamehe..
Kwakweli nilichanganyikiwa nakujiuliza hivi huyu binti anawezaje kutupanga wengi hivi..nilichofanya nikuchukua viatu nilivyokuja navyo nikamwambia nimejitoa kwenye hiyo cheni na kama viatu atakuleta mwingine hivi naondoka navyo.
Nipo njiani kurudi home massage za kuomba asemehewe na kuto rudia tena zinamiminika kwenye simu yangu huku akijuta na kudai mimi ndo ananipenda kiukweli nikimwacha hatopata furaha ya maisha nakuomba nimpe last chance abadirike…nikamjibu nakumwambia huwa natoa msamaha kwa makosa mengine lakini sio kwa hilo la kuchapiwa naomba tuachane kwa amani tu mama…akanipigia simu sikupokea akarudia tena na tena nikapokea..
Nikamuuliza unasemaje..akanimbia ananipenda sana na hawezi kuishi bila mimi uku akilia..nilichomjibu ni kwamba siwezi kuendelea nae.,
Kitu kingine kinacho nichanganya hapa nikwamba ametishia kujiua na yupo chini ya uangalizi wa dada yake..jamani hata kama ni msamaha nikifiria idadi yake ya wanaume nachefuka kabisa..napigiwa simu kila mara kuombwa nirudishe moyo na ndugu zake ninachowajibu ni kwamba siwezi ajaribu kumchagua mwingine atakayempenda sana..mpaka nafikia hatua ya kuwaandikia hii habari huyu binti amelazwa hospital presha imeshuka..
Hapa nafanyaje wakuu kiukweli huyu mwanamke amenitoka kabisaa..hofu yangu ni hiyo ya kulazwa kisa mimi inamaana nikigoma hata kwenda hospital..si ndio majanga yataongezeka..msaada wenu wakuu kichwa changu kimevurugwa kabisa.