NEWS

4 Septemba 2014

Diamond Platnumz Marufuku kufanya Show Ujerumani kwa hasara hii

Kufuatia vurugu zilizoibuka ukumbini alfajiri ya Jumapili iliyopita baada ya msanii Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kucheleweshwa kupanda stejini kwenye Ukumbi wa Sindelfingen uliopo Mji wa Stuttgart, Ujerumani, mwanamuziki huyo anadaiwa kupigwa marufuku kutia maguu nchini humo.



Kwa mujibu wa chanzo chetu makini mjini humo, ambacho pia kilikuwepo ukumbini wakati vurugu zilipoibuka, uchunguzi wa awali umeonesha kwamba, gharama ya vitu vilivyoharibiwa inakadiriwa kuwa zaidi ya Euro 128,322 sawa na Sh. milioni 280.

“Tukio la vurugu za Diamond limeripotiwa kwenye magazeti tofauti mjini hapa lakini kubwa ni hasira ambayo mashabiki wa Diamond wameionesha waziwazi.