NEWS

23 Septemba 2014

Huyu ndiye Mpenzi wa Hamisa Mabeto !


MAHABA niue! Mwanadafada ambaye ni mwanamitindo Bongo, Hamisa Mabeto ameamua kumwanika mwandani wake baada ya kumuweka kwenye mitandao ya kijamii huku akimmwagia sifa kemkem.



Akipiga stori na mwandishi wa gazeti hili baada ya kuvutiwa waya, Hamisa alisema mwanaume huyo ni mtu ambaye anampenda sana na wana malengo ya kuoana muda wowote kuanzia sasa na jina lake ataliweka hadharani soon!


Aliendelea kusema kuwa wana miezi sita mpaka sasa na amekuwa mtu ambaye anajua nini thamani ya mapenzi kwani muda wowote akimuhitaji anakuwa karibu yake.

“Ni kweli ni mpenzi wangu ambaye tunapendana sana na muda wowote kuanzia sasa tutafunga pingu za maisha kama mipango yetu ikikaa vizuri,” alisema Hamisa.