NEWS

21 Machi 2017

Forbes: Dangote Bilionea Namba 1 Afrika Mwaka 2017, Mo Dewji wa 20… Orodha Yote Ipo Hapa..!!!!


JARIDA Maarufu ambalo hufanya tafiti na kuchapisha rekodi mbalimbali za watu kwenye tasnia kadha wa kadha duniani, Forbes limemtaja Mfanyabiashara maarufu kutoka nchini Nigeria, Alhaji Aliko Dangote kuwa ndiye tajiri mwenye mkwanja zaidi barani Afrika akikadiriwa kuwa jumla ya $12.2 bilioni.

Kuna mabilionea (wa Dola) 25 mwaka huu barani Afrika, mmoja juu ya 24 waliokuwepo mwaka jana.

Wafanyabiasha kutoka Nigeria Femi Otedola na Abdulsamad Rabiu hawakufanikiwa kuingia kwenye orodha hiyo mwaka huu.

Mtanzania Mohammed Dewji bado ndiye bilionea wa umri mdogo zaidi Afrika, utajiri wake ukikadiriwa kuwa $1.09 bilioni.

Isabel dos Santos kutoka Angola na mfanyabiashara wa mafuta Folorunsho Alakija kutoka Nigeria ndiye mabilionea wanawake pekee katika orodha hiyo mwaka huu.

Bw Dangote Dangote, ndiye mwanzilishi na mwenyekiti wa kampuni ya Dangote Cement inayoongoza kwa kuzalisha saruji Afrika. Anamiliki asilimia 90 ya hisa za kampuni hiyo.

Dangote Cement huzalisha tani 44 milioni za saruji kila mwaka na imepanga kuongeza uzalishaji kwa asilimia 33 kufikia 2020.

Dangote pia anamiliki hisa katika kampuni za chumvi, sukari na unga.

Mohammed Dewji ni afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya METL iliyoanzishwa na babake miaka ya 1970. Kampuni hiyo huhusika katika biashara ya nguo, unga, vinywaji na mafuta. Kampuni hiyo huendesha shughuli zake katika zaidi ya mataifa sita barani Afrika.