NEWS

28 Februari 2018

Yanga: Subirini Ubingwa Mali Yetu

Wachezaji wa Yanga wakifanya mazoezi.

YANGA wamedai kwamba kikosi hicho ambacho wapinzani wao wanakibeza, basi kitabeba Kombe la FA na Ligi Kuu Bara kimiujiuza. Mwenyekiti wa Mashindano na Usajili wa Yanga, Hussein Nyika amewaambia mashabiki watulize mzuka hesabu zao wanazicheza kisayansi kwenye FA na ligi.

 

Yanga ambayo imetinga robo fainali ya FA huku ikishika nafasi ya pili katika ligi, kwa sasa inakabiliwa na majeruhi wengi kama Donald Ngoma, Thabani Kamusoko, Yohana Nkomola, Obrey Chirwa, Amissi Tambwe, Andrew Vicent ‘Dante’ na Abdallah Shaibu ‘Ninja’.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Nyika alisema wanapokea kejeli nyingi kutoka kwa wapinzani wao juu ya ubovu wa kikosi chao huku wakiamini wataukosa ubingwa kutokana na hilo, hivyo amewaondoa hofu Wanayanga katika hilo.

 

Nyika alisema ; “Tumesikia kejeli zao juu ya kikosi chetu kinachoandamwa na wachezaji wengi na muhimu waliokuwepo katika kikosi cha kwanza kukosekana katika baadhi ya mechi za ligi na kuponda kuwa hatuna timu ya ubingwa.”

 

“Sasa wao waache waendelee kutudharau lakini msimu huu sisi malengo yetu ni kuchukua Kombe la FA, kutetea ubingwa wa ligi na kwenye Ligi ya Mabingwa tufike hadi hatua ya makundi. Hicho ndiyo tunachokiangalia hivi sasa na kikosi hiki kibovu tulichokuwa nacho,”alisema Nyika

Stori na Wilbert Molandi

The post Yanga: Subirini Ubingwa Mali Yetu appeared first on Global Publishers.