WATU watano wakiwemo Soudy Brown, Shafii Dauda, Sudi Kadio, Benedict Kadege na Michael Mlingwa wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Septemba 24, 2018, wakikabiliwa na makosa ya kurusha maudhui kupitia Online TV bila ya kibali.
Washitakiwa hao walishuka kwenye karandinga la polisi wakitokea Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam walikokuwa wameshikiliwa huku wakiwa wamevalia kininja ili kuficha nyuso zao.

Kesi hiyo, ambayo kwa upande wa utetezi unawakilishwa na Wakili Peter Kibatala akisaidiana na wakili Maghimbi, Soudy Brown anashtakiwa kwa kosa la kurusha maudhui kupitia akaunti yenye jina la Shilawadu ambayo haijasajiliwa.
Shaffih Dauda na Ben Ali wameachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Septemba 24. Wawili hao wameshtakiwa kwa kuendesha blogu bila kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kosa ambalo wamekana mahakamani hapo. Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 8 kufuatia upelelezi kutokamilika.
VIDEO: TAZAMA TUKIO HILO HAPA
The post BREAKING: SOUDY Brown Alivyotinga Kortini Kisutu – Video appeared first on Global Publishers.