NEWS

30 Novemba 2018

Daimond Atoa Kwa Wazee Mkoani Iringa

Daimond Atoa Kwa Wazee Mkoani Iringa
TIMU ya Wasafi ikiongozwa na Mkurugenzi wake, Nasbu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na wasanii wenzake wamewasili jana mkoani Iringa kwa ajili ya maandalizi ya Tamasha la Wasafi Festival 2018 linalotarajiwa kufanyika leo Ijumaa, Novemba 30, 2018 katika Uwanja wa Samora mkoani humo.


Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza na Crew ya Wasafi Festival kabla ya utoaji msaada



Katika harakati za kuwasaidia wananchi wenye maisha magumu, Diamond na timu yake wamefika katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela na kuwakabidhi msaada wa vinywaji wazee wenye uhitaji maalum waliyofika eneo hilo leo.


Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Diamond amewahakikishia wananchi wa Iringa kufanya shoo ya nguvu itakayoacha historia katika Viwanja vya Samora.


Diamond ambaye ameongozana na wasanii wa muziki na Bongo Fleva wakiwemo Jackline Wolper, baada ya shoo hiyo watafanya Tamasha keshokutwa Jumapili mkoani Morogoro.


Aidha, Kasesela amempongeza Diamond kuwainua wasanii wachanga na wale wa zamani waliyokuwa wamepotea kwenye muziki na kumtaka endelee na moyo huo wa kuwasaidia na kufanya matamasha makubwa kama hayo kwenye maeneo tofauti.


Aidha, Mkuu huyo wa wilaya amemshauri Diamond kuwekeza kwenye kilimo kwani muziki utafika wakati atachoka (kuzeeka) hivyo mashamba/kilimo kitamuinua.