Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), limetangaza majina 34 ya wachezaji wanaowania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Kiume mwaka 2018. Pia kuna majina ya wachezaji 15 wa kike, wachezaji 6 vijana na makocha 10. Tuzo hizo zitatolewa Januari 8, 2019 jijini Dakar, Senegal.