Mbunge wa Chama cha Leba cha nchini Uingereza, Lloyd Russell-Moyle ametangaza hadharani kuwa anaishi na virusi vya UKIMWI
Moyle alitoa taarifa hizo jana Novemba 29, 2018 bungeni kwenye hotuba yake iliyokuwa yenye hisia nzito kuhusu Ugonjwa wa Ukimwi.
“Ninakaribia miaka 10 sasa tangu nipimwe na nikutwe na virusi vya UKIMWI nikiwa na miaka 22, lakini kwa kipindi chote nimekuwa msiri kuweka wazi afya yangu na kujikubali. Nimeumia sana hadi kufikia maamuzi haya ya kutangaza hadharani, kwa miaka yote nimekuwa najiona kichwa kizito kinachoshindwa kuchukua maamuzi hata pale nilipofanyiwa ushauri na watalaamu,“amesema Moyle.
Kwa siku ya jana, Baraza la Wawakilishi au Bunge nchini humo lilikuwa na mjadala mzito kuhusu kudhibiti ongezeko la wagonjwa wa Ukimwi duniani, hii katika kuelekea siku ya Ukimwi duniani hapo Desemba 1, 2018.
Moyle anakuwa Mbunge wa kwanza nchini Uingereza kutangaza hadharani kuwa anaishi na virusi vya Ukimwi. Tazama video yake hapa chini akizungumza
Hatua hiyo ya kutangaza hadharani imepongezwa na wabunge wenzake na wanaharakati kibao, wengi wakimuita kuwa ni shujaa.