Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda, anatarajiwa kuzipamba sherehe za kutimiza miaka 18 ya kituo cha Redio cha Magic Fm tangu kuanzishwa kwake.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Vipindi na Maudhui, Orest Kawau, amesema sherehe hizo zitafanyika kesho majaira ya saa tano asubuhi hadi jioni katika Viwanja Vya Shule ya Tandale hivyo kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi.
Pia amesema katika sherehe hizo kutakuwa na zawadi mbalimbali ambazo zitagawiwa kwa wasikilizaji wa kituo hicho cha Magic FM na kwa watakaowahi watajipatia zawadi maalum.
“Tumeamua kuadhimisha miaka 18 ya Magic FM ili kurudisha fadhila kwa wasikilizaji wetu ambao wametuunga mkono kwa kipindi chote tangu tulipoanza mpaka sasa. Tunawaomba watanzania waendelee kutuamini na tunaahidi kuwapa ladha inayostahili kwa wakati wote” Alisema Kawau.
Kwa upande wake Balozi wa Kampuni ya Bahati nasibu ya Daka Pesa ambao ni wadhamini wakuu wa hafla hiyo, Salum Salehe, amesema kampuni imeamua kudhamini sherehe hizo ili kuungana na kituo hicho hasa katika kutoa elimu juu ya huduma wanazotoa kupitia mchezo wao wa Daka Pesa ambapo mteja anaweza kucheza kwa kiwango cha kuanzia 500 na kujishindia zaidi ya milioni 1.
The post RC MAKONDA KUPAMBA SHEREHE ZA MIAKA 18 YA MAGIC FM KESHO, TANDALE appeared first on Global Publishers.