STAA wa filamu za Kibongo, Ester Kiama ameibuka na kudai kuwa anatamani siku moja naye ateuliwe kuwa mkuu wa wilaya na anayemtamanisha ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo.
Akizungumza na Risasi Jumamosi, Ester alidai kuwa, kwa sasa Jokate amekuwa ‘role model’ wake na anaamini siku moja atakuwa kama yeye.
“Unajua nimejikuta natamani kuwamkuu wa wilaya flani hivi ingawa najua siyo mchezo kama watu wanavyofikiria. Kiukweli Jokate ndiyo amenifanya nitamani hivyo, navutiwa na utendaji kazi wake lakini pia anavyonyuka zile suti. Na mimi nimeshaanza kumuiga katika uvaaji,” alisema Ester.
Usichokijua kuhusu Mpenzi Mpya wa DIAMOND
The post ESTER KIAMA ATAMANI CHEO CHA JOKATE appeared first on Global Publishers.