Msanii wa muziki wa kizazi kipya African Princess maarufu kama, ‘Nandy’ ameonyesha zawadi ya nyumba aliyowajengea wazazi wake kwa mwaka 2018 ambayo inapatikana maeneo ya Dar Es Salaam.
Kupitia akaunti yake ya instagram ameweka kipande cha video na picha ambazo zinaonyesha nyumba hiyo na maelezo yanayosomeka, “Mungu wangu na Baba yangu najua nakukosea sana kama binadamu na kama kijana ila nikipiga goti unajua namaanisha kutoka moyoni mwangu na unajua hakuna ninaye mtegemea zaidi yako… Asante kwakunipa uvumilivu, unyenyekevu, katika maisha yangu hasa kipindi hiki cha mwaka 2018!! Asante kwa hii zawadi ndogo ya wazazi wangu najua hii ni ndoto ya kila kijana mwenye kutafuta!!! Ni kila ndoto ya mwanadamu yoyote duniani kuona wazazi wake wako na furaha na ndiyo baraka zenyewe” .
Aliendelea kwa kuchukua nafasi ya kutoa shukrani zake kwa kuandika, “Nashukuru media zote , blogs zote, ma producers wote, ma promoters wote, familia yangu ya THT, familia yangu ya clouds ,management yangu, Team yangu, marafiki zangu, Baba yangu wa kiroho Mtumishi MWAMPOSA , na mafans wangu wote ,bila kusahau na hatters wote kwa kunipa nguvuu na supports kwa namna moja au nyingine uwepo wenu ndio mafanikio yangu……..
Nili jipa nguvu kabla sijapewa
Nilijipa moyo kabla sijapewa
Nilijiamini kabla yakuaminika
Nilijikubali kabla yakukubalika
Popote ulipo kijana mwenye ndoto yoyote ile jua inawezekana ukiweka nia ukikubali mazuri na mabaya yote yakufikie sababu ni daraja na nguzo ya mafanikio yako bila kusahau MUNGU ndio kila kitu. Nawapenda
HAPPY NEW YEAR IN ADVANCE
#DADAMWENYENYUMBA”
TAZAMA VIDEO HAPA
Nyumba Ya Nandy
null
Post nyingine ilikuwa ina maelezo yanayosomeka, “A small gift for my parent this year 2018…
Zawadi ndogo ya wazazi wangu mwaka huu 2018..”
Msanii mwingine pia aliyetoa zawadi ya mkwanja mrefu kwa wazazi wake mwaka huu ni msanii Dogo Janja ambaye alimjengea mama yake nyumba huko Arusha.
The post Zawadi Ya Mamilioni Nandy Aliyowazawadia Wazazi Wake Mwaka 2018 (Picha & Video) appeared first on Global Publishers.