NEWS

31 Desemba 2018

Kuokoka Kwa Amber Rutty Gumzo

Mchungaji Emmaus Bible Church lililopo Mbezi-Luis jijini Dar akiwa na Amber Rutty.

Video Queen Mus­cat Abubakary ‘Amber Rutty’ na mpenzi wake Said Bakary Mtopali wamedaiwa kuokoka kitendo kilichozua gumzo kwa watu kutokana na awali baba wa Amber Rutty kumjia juu mchungaji Dau­di Mashimo na kudai kuwa mtoto wake huyo hawezi kuokoka.

 

Gumzo hilo limeibuka baa­da ya kubainika kuwa Amber Rutty na mpenzi wake kuwa karibu na mchungaji Mash­imo huku ikielezwa kuwa wanaishi kwenye nyumba ya kanisa la mchungaji huyo li­itwalo Emmaus Bible Church lililopo Mbezi-Luis jijini Dar.

 

“Huyu Amber Rutty anawe­zaje kuokoka wakati ni muislamu, kwani kusaidiwa na mchungaji ndio lazima aokoke, halafu nasikia ataan­za kuimba kwaya makubwa haya jamani,” kilisema chan­zo kilichowaona wawili hao wakiongozana na mchungaji Mashimo kanisani kwake.

 

Kama hiyo haitoshi, hivi karibuni wapenzi hao walionekana nyumbani kwa muimba Injili, Dk. Wema Shamshama, maeneo ya Goba jijini Dar aliyefiwa na mumewe ambapo wal­ipokelewa vyema na baadhi ya waimba Injili kama Em­manuel Mbasha na Bahati Bukuku.

 

Mbasha alipoulizwa na mwanahabari wetu ana­wachukuliaje wapenzi hao ambao wamezua gumzo kutokana na kuokoka kwao, alisema kuwa yeye kama mlezi wa waimba Injili, ame­wapokea kwa mikono miwili na kwamba iwapo watataka msaada wowote atawapatia ikiwa ni pamoja na kuimba nao Injili kwani anaamini kuwa kila mwanadamu ana makosa yake na akitubu anasamehewa.

 

“Nimefurahi kusikia wamempokea Kristo pen­gine Mungu alitumia njia ya kuwasababisha wapitie aibu na fedheha ili moyo wa unyenyekevu uumbike ndani yao na kufanya iwe rahisi kwao kuupokea wokovu wa Bwana wetu Yesu Kristo, nikiwa kama baba wa kiroho na mlezi mkuu wa waimbaji wote wa nyimbo za Injili Tanzania, ninatoa angalizo kwa Amber Rutty pamoja na mwenzake, ingekuwa vyema sana kwao kukaa chini na kujifunza kwanza pasipo kukimbilia kufanya huduma yoyote, ili wapate muda wa kulelewa na kukua kiroho kwanza kisha nitawasaidia pale watakapokuwa na uhitaji hasa kwenye suala la kuimba,” alisema Mbasha.

 

Amber Rutty na mpenzi wake wanakabiliwa na mashtaka matatu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar yakiwemo ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile na kusam­baza picha za ngono kupitia mitandao ya kijamii ambapo kesi yao bado inaendelea kuunguruma na sasa wako nje kwa dhamana.

Kabla ya dhamana hiyo wawili hao walisota ka­tika Gereza la Segerea kwa takriban siku 26.

Stori: Hamida Hassan

The post Kuokoka Kwa Amber Rutty Gumzo appeared first on Global Publishers.