NEWS

2 Januari 2019

Azam TV Yaileta FA Cup Kwa Kiswahili

KAMPUNI ya Azam Media Group kupitia Azam TV, itaonyesha matangazo ya mechi zote za michuano ya The Emirates FA Cup ya nchini England kwa Lugha ya Kiswahili.

 

Hatua hiyo imekuja baada ya kampuni hiyo kupata kibali cha kuonyesha michuano hiyo mikongwe na yenye historia kubwa nchini England.

 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar, juzi Jumatatu, Mtendaji Mkuu wa Azam Media Group, Tido Mhando, alisema: “Desemba 2018, tumefikisha miaka mitano tangu kuanzishwa kwa Azam Media Group, hivyo tunafarijika kwa muda wote huo kuwa sehemu ya kuwapa burudani watazamaji wetu hususani wale wanaofuatilia soka.”

 

ya The Emirates FA Cup ambayo ina takribani miaka 150 tangu kuanzishwa kwake, tunaamini watazamaji wetu wataendelea kufurahia kile ambacho tumekuwa tukiwapa.

 

“Kikubwa ambacho naweza kuwaambia ni kwamba, matangazo haya yatawajia kwa Lugha ya Kiswahili tena yenye vikorombwezo kibao kama ambavyo tunavyofanya kwenye La Liga, lakini pia mtazamaji atakuwa na uwezo wa kuchagua Lugha ya Kiswahili au Kingereza kupata matangazo hayo.

 

“Tumepewa haki za kuonyesha mechi zote za michuano hii kwa muda wa miaka mitatu, hivyo basi kuanzia Januari 4, mitanange hiyo itaanza kuonekana kwenye chaneli zetu na ikitokea siku kuna mechi nyingi kwa wakati mmoja, basi chaneli zetu zote zitaonyesha mechi hizo, yaani bandika bandua.”

“Kupitia chaneli zetu zilizopo Azam TV, tunapenda kuwaambia kuwa tutaonyesha michuano

The post Azam TV Yaileta FA Cup Kwa Kiswahili appeared first on Global Publishers.