VIDEO mixen ambaye anatamba hapa Bongo, Zena Abdallah ‘Jike Shupa’ ameapa kumlea mwanaye ajaye katika maadili ya Kidini.
Wakati mwingine mipango kabla ya tukio ‘inamata’, maana Jike Shupa amejiapiza hivyo miezi minne kabla ya kujifungua kwake, ambapo amesema, akizubaa katika malezi mwanaye ajaye anaweza kufuata mkumbo wa maisha mabaya.
“Natarajia kujifungua mwezi wa nne Mungu akipenda, sijaenda kupima ili nijue nitajifungua mtoto wa jinsia gani, lakini natarajia siku za hivi karibuni nifanye hivyo kwa kuwa natamani nijue nimebeba kiumbe cha jinsia gani,’’ alisema Jike Shupa.
NEEMA ADRIAN
The post Jike Shupa aapa kumlea mwanaye kidini appeared first on Global Publishers.