NEWS

1 Januari 2019

Baraka da Prince na Naj Kufunga Ndoa Mwaka Huu

Baraka da Prince na Naj Kufunga Ndoa Mwaka Huu
Msanii wa Bongo Fleva, Barakah The Prince ameweka wazi kuwa mwaka huu atafunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi, Naj.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake unaokwenda kwa jina la Furaha ameeleza kuwa atatimiza hilo kama ahadi yake kwa mpenzi wake huyo.

Utakumbuka mwaka uliomalizika Barakah The Prince aligonga vichwa vya habari mara baada ya kubadilisha dini, baadhi ya taarifa zilidai kuwa msanii huyo amefanya hivyo kutokana na shinikizo kutoka kwa Bibie madai ambayo Barakah aliyatupilia mbali.