Kitengo cha jeshi la Marekani kinachosimamia silaha za kinyuklia, kimeomba msamaha kwa ujumbe uliotumwa katika mtandao wake wa twitter uliosema kuwa kitengo hicho kilikuwa tayari kuangusha bomu kubwa zaidi ya New York's Times Square ball.
Ujumbe huo uliotumwa mkesha wa kuamkia mwaka mpya uliandamana na kanda ya video inayoonyesha ndege ya kivita aina ya B-2 Bomber ikiangusha silaha.
Kitengo hicho baadaye kilifuta ujumbe huo kikisema kuwa haikuwalengo lao na kuubadilisha na msamaha.
Yesu Kristo muonekano wake ulikuwa vipi?
Miji ilivyoukaribisha Mwaka Mpya wa 2019
Rais Duterte asema alimnyanyasa kingono yaya
Kisa hicho kilizua hisia kali katika mitandao ya kijamii.
Ulichapishwa katika mtandao wa kijamii saa chache kabla ya kuangushwa kwa mpira huo mkubwa juu ya One Times Square, ambalo ni jengo refu la mjini New York, ili kuadhimisha kuanza kwa mwaka mpya.
Ujumbe huo wa Twitter uliofutwa ulizua hisia kali
Wakosoaji walishutumu kwa haraka tukio hilo la kitengo hicho cha jeshi.
Aliyekuwa kiongozi wa afisi ya maadili nchini Marekani Walter M Shaub Jr. alituma ujumbe wa twiter akisema: Ni watu gani wanaoendesha taifa hili?
Joe Cirincione , mtayarishaji wa Nuclear Nightmare, kuimarisha usalama duniani alisema: Kwanza sikuamini kwamba hili litafanyika. lakini limefanyika.
''Ni mzaha mbaya wa kitengo cha kusimamia silaha za nyuklia. Ni aibu''.
Kitengo cha kusimamia silaha za kinyuklia nchini Marekani ni mojawapo ya vitengo 10 katika idara ya ulinzi nchini humo.
Makao yake ni kambi ya wanahewa ya Offtutt mjini Nebraska. Kauli mbiu yao ni ''amani ni taaluma' ambayo pia ilitumika katika ujumbe huo uliozua utata.