KIPA namba moja kwa sasa wa klabu Yanga, Ramadhani Kabwili, amefunguka kuwa kipa mwenzake Benno Kakolanya atarejea hivi punde kujiunga na timu hiyo.
Kabwili ndiye kipa kinara kwa sasa katika klabu hiyo ambapo amekuwa akisaidiana na Klaus Kindoki baada ya Kakolanya kuwa nje.
Akizungumza na Championi Jumatano Kabwili amesema anamuomba Mungu aendelee kumpa uvumilivu Kakolanya kwa kuwa haya yoyote yatapita na punde atarejea kikosini kujiunga na wenzake.
‘’Najua Kakolanya atarejea kikosini muda siyo mrefu kwa kuwa sisi wachezaji na timu bado tunamuhitaji, namuomba tu kaka yangu awe mtulivu kwa sababu najua kila kitu kitakuwa sawa na atarudi tuipiganie timu yetu ili tuweze kuchukua kombe msimu huu.
“Tuna kocha mwenye uelewa mkubwa sana, najua kuwa kuna siku atamsamehe, nami naomba sana iwe hivyo,’’ alifunguka Kabwili.
The post Kabwili Amuombea Kakolanya Yanga appeared first on Global Publishers.