NEWS

2 Januari 2019

Kauli ya Dkt. Bashiru yamuibua Mwigulu Nchemba

Kauli ya Dkt. Bashiru yamuibua Mwigulu Nchemba
Mbunge wa Iramba Magharibi, Dkt. Mwigulu Nchemba ameunga mkoni msimamo wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),  Dkt. Bashiru Ally kuwa muda wa kampeni ndani ya chama hicho ni bado kwa sasa.

Dkt. Nchemba amesema kuwa kulikuwa kumeshaanza kujitokeza magenge ndani ya chama na wengine kuhujumu uongozi katika utekelezaji wa Ilani ya chama hicho ila kauli ya katibu mkuu huyo imeweka kila kitu sawa.

"Ujumbe Murua, magenge yameibuka, wengine hata utekelezaji wa Rais na Ilani wanageuza ni kazi zao, utawasikia nimetumwa kugombea na Mwenyekiti na Katibu Mkuu." ameeleza Dkt. MWigulu kwenye mtandao wa Twitter.

Ameendelea kwa kusema, 'Na wengine vikao vya siri kuhujumu viongozi na ilani ya CCM, asante kwa kuweka wazi msimamo wa chama