NEWS

2 Januari 2019

Moni Hapendi Niwe na Mabifu Mtandaoni”- Nai

Moni Hapendi Niwe na Mabifu Mtandaoni”- Nai
Video vixen maarufu kwenye tasnia ya Bongo fleva Nai amefunguka na kuweka wazi kuwa mpenzi wake ambaye ni staa wa Hip hop nchini Moni Centrozone hapendi akiona ana mabifu kwenye mitandao ya kijamii.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Nai alisema huwa analazimisha tu kuwajibu wanaomsema vibaya mitandaoni, lakini ukweli ni kwamba mpenzi wake huyo hapendi na amekuwa akimkataza mambo hayo mara kwa mara.



Katika vitu ambavyo mpenzi wangu Moni hapendi ni mimi kuwa na ugomvi na wenzangu hasa mitandaoni. Huwa anakereka sana na mara nyingi amekuwa akiniambia nikae kimya, lakini kuna wakati nashindwa kuvumilia matusi na maneno mabaya ambayo nakuwa naambiwa na baadhi ya watu wasiopenda maendeleo yangu, hivyo najikuta nimewajibu ili na mimi nafsi yangu iridhike”.

Siku chache zilizopita Nai aliingia kwenye Bifu kali na video vixen wengine kama Mke wa Rayvanny maarufu kama Fahyvanny na rafiki yake Official lynn.