NEWS

1 Januari 2019

Nimegundua Ana Mimba ya mtu Mwingine Baada ya Kumchumbia na Kunikubalia Kumuoa



Salaam zetu, habari hizi zinanisikitisha kidogo ,kijana mmoja ambaye ni mtu wangu wa karibu , amekuja kuniomba ushauri Na maelezo yake yako hivi

"Miezi kadhaa iliopita nilikutana Na msichana Mrembo anasoma chuo, lakin Alikuwa akimaliza masomo yake ya diploma, tukawa tumekuwa marafiki ,nikawa nami nasafiri kwenda mkoani kwa siku 14, lakin nikiwa uko uko mkoani nikaamua kumu approach kupitia mawasiliano akasema ni vema nikirudi ndo tukae tuzungumze, nikarudi toka mkoani tukakutana hotelin tukazungumza kwa Kina ,nilimuelezea mipango yangu ya kwanini nataka niwe naye kwa mahusihano, naye akakubali, tukawa wapenzi kabisa.

Nikawa namuita tunakutana tunaongea habari mbali mbali. Bila kishiriki tendo la ndoa,

Sasa baadae wiki Jana amenipigia simu kuwa ninaomba nikwambie Jambo please, nkasema sawa akasema naomba usishtuke nataka kukwambia lakin naogopa, nkasema kuwa huru akasema mpenzi Nina mimba ya mvulana tuliyeachana ambaye nimekueleza Na ina miez 2, kwakweli nimepigwa Na butwaa ni msichana Mrembo nampenda, nimeshawajulisha hadi wazazi wanamjua, Sijawahi shiriki naye tendo la ndoa kwa kusema ngoja nisubiri tuoane,
Baada ya kunambia nilivuta pumzi nikakaa kimya kidogo nkasema tuwasiliane baadae, nikawazaaa, sasa ananambia mimba aitoe kwa kutumia madawa ya kichina, ambayo yanaharibu mimba inatoka kama damu,
Sasa najiuliza ndugu yangu
1. Je hayo hayataaribu kizazi kamwe hakose mtoto tukiwa wote mbeleni?
2. Zambi za mtoto huyu hazitatutafna? Maana ukiua lazima IPO siku utajutia uamzi UO,
Nimeenda kwa marafiki zangu wakasema haina shida mpe elfu 60 atoe, lakin mmoja akasema kwanza nenda naye hospital uhakikishe maana wasichana siku hizi wajanja mno, Anaweza kukupiga hela TU, tumeenda kwa Dokta ni kweli Ana mimba , mbaya zaid dokta kanipongeza Mimi kwamba hongera mkeo Ana mimba,
Nifanye nini? "

Mwisho wa kunukuu anaomba ushauri, this is true story

By Venchwa