NEWS

2 Juni 2019

Rais wa CAF aitisha kikao cha dharura

Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika CAF, Ahmad Ahmad ameitisha kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo kufuatia sintofahamu katika mchezo wa pili wa fainali ya Klabu Bingwa Afrika.

 

ES Tunis wakishangilia ubingwaMchezo huo ambao ulifanyika Ijumaa, Mei 31 nchini Tunisia kati ya wenyeji Esperance de Tunis na Wydad Casablanca ya Morocco uliisha kwa sintofahamu kufuatia klabu ya Wydad kugomea kuendelea na mchezo baada ya bao lao la kusawazisha kukataliwa katika dakika ya 62 ya mchezo.

 

Taarifa ya CAF imesema kuwa kikao hicho kitafanyika Juni 4, ambapo ajenda kuu itakuwa ni juu ya sheria zainazopaswa katika kutatua sintofahamu ya mchezo huo.kwenye mchezo huo, Wydad walisawazisha bao, ambalo lingeufanya mchezo kuwa sare ya 1-1 lakini mwamuzi alikataa bao hilo na halikurudiwa katika teknolojia ya usaidizi wa video VAR kwa kile mwamuzi alichokidai kuwa mashine kuharibika.

 

Baada ya Wydad kugoma kuendelea na mchezo, mwamuzi alimaliza mchezo na kuipa ushindi wa bao 1-0 klabu ya Esperance pamoja na ubingwa wa michuano hiyo.

Tazama SHIGONGO Alivyofuturisha YATIMA, Ma Sheikh Wamwaga Dua!

The post Rais wa CAF aitisha kikao cha dharura appeared first on Global Publishers.