NEWS

2 Juni 2019

Wabunge Wenye Nongwa CCM waonywa na Pole Pole


CCM imesema wabunge wa chama hicho aliowaita wenye nongwa  kila Serikali inapotatua matatizo mbalimbali, ikiwemo kununua korosho watakuwa na hali ngumu 2020.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole ametoa kauli hiyo leo katika mahafali ya wanafunzi wanachama wa CCM wanaotarajiwa kumaliza elimu ya juu mkoani Mtwara, Ambapo amewataka Wabunge kutafuta kazi nyingine.

Amesema wabunge wanaofanya hivyo wanapaswa kujipanga mapema, “Kama wewe ni CCM na unashiriki nongwa kwa jambo hili ambalo tumelifanya kwa uchungu mkubwa jipange mapema.”

“Jipange kwa sababu mimi na wenzangu kuanzia sekretarieti, kamati kuu na halmashauri kuu tupo kitu kimoja tumeweka mustakabali sawa kulinda utu na heshima ya wakulima.”