NEWS

31 Julai 2019

Kisa cha Pili Cha Ebola Chathibitishwa Kwenye Mji wa Mpakani mwa Kongo wa Goma


kisa cha pili cha ugonjwa wa Ebola kimebainika katika mji wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo unaopakana na Rwanda, kikiibua hofu ya kuwa ugonjwa huo unaoua unaweza kusambaa.

kisa hicho kilithibitishwa katika mji wa Goma, unaokaliwa na watu milioni mbili, maafisa wanasema.

Zaidi ya watu 1,600 wamekwisha kufa kutokana na Ebola katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo tangu mlipuko wa ugonjwa huo ulipotokea Agosti 2018.

Shirika la Afya duniani wiki iliyopita lilitangaza mlipuko wa ugonjwa huo kama dharura ya dunia ya afya.


Ni kiwango cha juu cha sauti ya dharura ambacho WHO linaweza kuitoa na imewahi kutolewa mara nne tu awali - ukiwemo mlipuko wa Ebola uliowakumba watu wa Afrika Magharibi kuanzia mwaka 2014 hadi 2016, ambao uliwauwa zaidi ya watu 11,000.

Hali ikoje katika mji wa Goma?

Ebola inaathiri majimbo mawili ya Kongo - kivu Kaskazini na Ituri. Goma ni mji mkuu wa jimbo la kivu Kaskazini na Unapatikana katibu tu na mji wa mpakani wa taifa jirani la Rwanda wa Gisenyi.

Kasisi mjini Goma alikufa kutokana na ugonjwa wa Ebola mapema mwezi huu .

Jumanne , Dr Aruna Abedi - ambaye anaratibu shughuli za huduma za uhgonjwa huo katika jimbo la Kivu Kaskazini aliliambia shirika la habari la AFP kuwa amefahamishwa kuhusu kisa cha pili cha Ebola.

"Hatua zote zimechukuliwa ili mgonjwa aliyepatikana ahudumiwa mjini Goma," imesema taarifa rasmi.

Ramani inayoonyesha mataifa ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Goma, na Rwanda
Eneo hilo linakaliwa na idadi kubwa ya watu na kuna hofu kuwa hii inaweza kusababisha kusambaa kwa ugonjwa huo hadi ndani ya Rwanda.

Ingawa katika nchi hiyo hakuna kisa cha Ebola kilichokwisha thibitishwa , tayari nchi hiyo imekwishajiandaa kwa kuweka vituo vya matibabu ya Ebola na inaandaa vituo vitatu vya kuwatenga watu watakaopatikana na maradhi hayo hatari pindu kisa chochote kitakapojitokeza.

''Rwanda imefanya juhudi kubwa za kuwekeza katika maandalizi ya Ebola'' Alisema mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt Tedros Adhamon Ghebreyesus wiki iliyopita.

"Lakini kama mlipuko wa Ebola unaendelea katika jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, kuna hatari kubwa halisi ya kuenea katika nchi jiran