NAJUA ulikuwa ukijiuliza sana eti mbona shoo za mwanamitindo na msanii mpya wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto huzioni! Jibu hili hapa; Kwa mara ya kwanza Uwanja wa Taifa wa Burudani Dar Live uliopo Mbagala- Zakhem jijini Dar unatarajia kumshusha Hamisa na wakali wengine kibao katika Sikukuu ya Eid al Hajj (Agosti 12). Akizungumza na Showbiz, mratibu wa Dar Live, Rajab Mteta ‘KP Mjomba’ alisema tamasha hilo limepewa jina la Bonsi Vibe likimaanisha Usiku wa Bongo Fleva na Singeli.
“Litakuwa tamasha la aina yake kwani Mobeto hajawahi kupafomu shoo ya wazi na hii itakuwa mara ya kwanza katika Viwanja vya Dar Live, siku hiyo warembo wote, mashabiki, wanamitindo na wadau wa muziki watahamia Dar Live sijui wewe utakuwa upande gani,” alisema KP.
Mbali na uwepo wa Mobeto atakayeimba live kwa kutumia vyombo nyimbo zake zote kali kuanzia My Love, Tunaendana na Sawa, jukwaa pia litashambuliwa na Mr Blue, Chid Benz, Pam D, Mzee wa Bwax huku kundi la matarumbeta likiongozwa na Kiroboto OG likifanya yake. Tamasha zima litakuwa kwa kiingilio kiduchu kuliko unavyodhania kwani kwa buku tano tu yaani 5,000 utapata burudani zote hizo
The post MOBETO NDANI YA DAR LIVE appeared first on Global Publishers.