NEWS

31 Julai 2019

Tatizo hawa wadukuzi hawachukuliwi hatua- Bernard Membe



Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa awamu ya Nne, Bernard Membe, amesema sauti zilizovuja hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii ikihumusisha yeye akifanya mazungumzo na mtu asiyefahamika wakijadili juu ya sintofahamu ndani ya CCM ni ya kwake.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na vyombo habari, ambapo amesema kuwa ni kweli sauti iliyodukuliwa na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii ni ya kwake asilimia 100 huku akiomba Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuingilia kati suala hilo.

“Sauti ni za kwangu ni mimi 100 kwa 100, na nimeifanyia kazi na ninajua imetoka wapi kwa sababu nina miiko ya kuzingatia sisemi, Ni sauti yangu kabisa na ninaelewa kila kilichotokea unaweza kuingia ugonjwa wa udukuzi, kama wale wanaotoa taarifa hizi za udukuzi hawachukuliwi hatua, wadukuzi wako duniani wanataka fedha tu,”amesema Membe.
Read More:Nafasi za Ajira 291 Zilizotangazwa Leo  

Hivi karibuni IGP Simon Sirro alisema kuwa wanafuatilia suala la sauti hizo na endapo wakigundua kuna kosa la jinai wahusika watafikishwa mahakamani.