UKIFIKA katika Jiji la New York kuna jarida moja maarufu la urembo na mitindo linalotoka kila mwezi ambalo ndani yake llinachukua Wamarekani weusi au Waafrika wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 49. Jarida hilo limekuwa maarufu kutokana na kupamba kwa mastaa wakubwa wa filamu na muziki ambao wamekuwa wakiingia hadi kwenye mitindo kama vile Usher Raymond, Taraj P. Henson, Alicia Keys, Michelle Obama, Rihanna na wengine wengi. Kwa mara ya kwanza jarida hilo lilifanya mahojiano na staa wa muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ na kumpambia katika kurasa zake ndani.
Ukiachana na hilo, jarida jingine maarufu Afrika la Tush ambalo linatokea katika nchini Nigeria nalo lilifuata nyayo za Essence za kumtumia Vee Money ambapo lilimpamba katika ukurasa wake wa mbele likimuelezea namna anavyoupeleka muziki wa Bongo Fleva kwenda duniani.
Yes! Vee Money ni mwanamuziki wa kike anayekimbiza katika muziki wa Bongo Fleva kimataifa, mbali ya kufanya kolabo kadhaa za kimataifa na wakali kama K.O wa Afrika Kusini na pacha wa P Square, Peter Okoye ‘Mr.P’. Vee Money amekuwa pia akijichanganya na mastaa wengi kutoka Marekani akiwemo Trey Songz.
Hata katika jarida hilo, mara baada ya kufanyiwa mahojiano alipata mualiko wa kwenda nchini Marekani katika tamasha lao kubwa ambalo lilikuwa na mastaa kibao kama Nas, Mary J Blige, Timbaland, Mase, Brandy na Miss Elliot.
Kwa sasa Vee Money ambaye ana ratiba ya shoo za kutosha ndani na nje ya nchi hadi Desemba, mwaka huu, ameachia albamu yake ya nyongeza ‘EP’ inayokwenda kwa jina la Expensive. Chini ni mahojiano yake aliyoyafanya kupitia The Playlist chini ya mtangazaji Omary Tambwe ‘Lil Ommy’.
VEE MONEY: Ulijisikiaje ulipopata mualiko wa Jarida la Essence Marekani?
RISASI VIBES: Ilikuwa kama ndoto kwani wiki chache zilizopita walikuja Zanzibar walikuwa wana ‘shoot’ wakatafuta wasanii ambao watakuwa kwenye hiyo shoo, wakanipata mimi na Magesse ni baraka kubwa sana kwangu kuwa msanii wa kike kutoka Tanzania na Afrika Mashariki.
VEE MONEY: Muziki wa Bongo nchini Marekani wanauchukuliaje?
RISASI VIBES: Wamarekani sasa hivi wana masikio ya kusikiliza muziki wa nje ni kuamua sisi wenyewe kama Waafrika ambao ni waandaaji wa matirilio kuchukua hii fursa kama nafasi ya kupenyeza kwenye soko la kimataifa.
RISASI VIBES: Wabongo tunafeli wapi kushindwa kujulikana sana kimataifa?
VEE MONEY: Wenzetu wanavyoitambua miziki yetu ni Afro Beats sisi tupo katika Afro Pop utaona ni chini ya mwavuli uleule, Naija Music na mingineyo lakini wenzetu huwa wanashindwa kutofautisha kati ya Afro Beats na muziki wa Lingala, Dansi na mingine mingi.
Tunahitaji soko kubwa la kimataifa kwani wanunuzi wa kazi za muziki Afrika ni wachache sana.
RISASI VIBES: Kuna kipindi Chris Brown aliku-follow Instagram ulishawahi kuwasiliana naye kabla?
VEE MONEY: Yaani sijui hata alini-follow lini kwani kuna shabiki wangu tu aliniambia Chris ameni-follow ninachokumbuka ni kitu kimoja tu niliwahi kufanya naye shoo Nairobi miaka miwili au mitatu iliyopita tukiwa na Wizkid na Alikiba.
RISASI VIBES: Kuna siku uliwahi kuachia picha ya Fally Ipupa katika ukurasa wako wa Insta lakini siku hiyo kesho yake Diamond akaachia video akiwa naye, ulikwazika kwa hilo?
VEE MONEY: Nilikuwa ninatamani kufanya naye kazi siku nyingi. Kwa miaka mitatu iliyopita niliwahi kuwasiliana na meneja wake anaitwa Madina akaniambia kwa sasa yupo bize anafanya albamu yake nikachukulia kama ameniambia No. Lakini kama zali nikakutana na Fally, Ufaransa kwa kuwa siyo mtu anayependa kutumiwa nyimbo nikatafuta fursa hiyo kufanya anavyotaka yeye thanx God nimefanikisha. Sitaki kuamini kama Diamond kutangulia kwake kuachia wimbo imenikwaza lakini kila kitu ni muda unaopangwa na Mungu.
Risasi Vibes: Lakini kuna siku ulikutana na Mb’ilia Bel ukaweka picha na kusifu vipi kuna kinachoendelea?
VEE MONEY: Nampenda sana Mb’ilia na huwa namzungumzia mara kwa mara namchukulia kama Madonna enzi. Nilionana naye kimasihara tu tukaongea naye basi.
RISASI VIBES: Kuna siku uliposti mtandaoni umeshuka kwenye ndege ukaongea not Made in China ulikuwa unamaanisha nini?
VEE MONEY: Nilikuwa nazungumzia mashairi ya wimbo wa Wande Cool sasa watu wakaanza kuweka vitu vyao lakini ilikuwa mahojiano kati yangu na wenzangu.
RISASI VIBES: Idea ya Moyo inaonekana zaidi ya kitu ulichokifanya lakini video yako kama unakimbia unatazama nyuma ulikuwa unamaanisha nini?
VEE MONEY: Watu wengi wananiambia mbona vitu vingi haviuunganiki kwenye hiyo video ni kwamba moyo una kazi nyingi, unapitia vitu vingi hofu, uoga, kukimbizwa na wakati mwingine unakuwa mweupe unatulia, wakati mwingine unafanya vitu hadi unashangaa. Hapo ninapokimbizwa ni kazi zangu za muziki sitaki kurudi nyuma.
RISASI VIBES: Wewe na mwanamitindo Huddah mnapenda kuitana mke mwenza kivipi hapo?
VEE MONEY: Kuna kipindi ilisemekana anatoka na Juma (Jux) tukawa tunaitana mke mwenza.
RISASI VIBES: Umeshawahi kuonekana na Hashim Thabeet kwenye Insta live ukasema utamwambia kwa meseji, ukaribu wenu upoje?
VEE MONEY: Hivi hamjui kama Hashim ana mke. Hashim ni mshikaji wangu tangu naanza kufanya muziki, amekuwa akinisapoti kwa miaka mingi na mimi namsapoti. Alipoenda live anajua mimi ni mshikaji wake siwezi kumfanyia ujinga kama ingekuwa nimeingia live na Serena Williams isingekuwa stori najua.
RISASI VIBES: Una mpango wa kupata mtoto kwa sasa?
VEE MONEY: Natamani sana lakini siku ikifika itaongea.
The post VEE MONEY ANAZIDI KUIPELEKA BONGO FLEVA KIMATAIFA appeared first on Global Publishers.