MSANII wa Bongo Fleva, Baraka Andrew ‘Baraka The Prince’ amesema anajivunia kuwa na mpenzi wake wa sasa,Naj kwa sababu ni msichana mrembo na mwenye mvuto machoni pa watu wengi ambaye ana maadili mema na ndiyo maana hata penzi lao limedumu tofauti na alipokuwa katika uhusiano na Nisha pamoja na Meninah.
Akizungumza Showbiz Xtra, Baraka alisema kuwa anafurahi sana pindi anapokuwa faragha na mrembo huyo, mithili ya kujiona kama yupo ‘peponi’ kwani ni mtu aliyefundwa na akafundika.
“Najma bwana sijui nimuongelee vipi, lakini ukweli ni kwamba nikiwa naye huwa siwakumbuki kabisa ma– ex wangu, yaani hapa hakuna cha Nisha wala Meninah kawaburuza wote. Anajua kubembeleza acha tu, yaani muda mwingine ana mapenzi mpaka naogopa, hivi nasubiri tu kumuweka ndani ndio nafsi yangu itaridhika,” alisema Baraka.
The post BARAKA THE PRINCE: NAJ kawazidi Nisha, Meninah appeared first on Global Publishers.