NEWS

3 Agosti 2019

China yaahadi kulipa kisasi dhidi ya ushuru wa Marekani

China imesema  inajitayarisha kuchukua hatua za kulipa kisasi iwapo rais Donald Trump wa Marekani ataendelea na mipango yake ya kuongeza ushuru kwa bidhaa za China zenye thamani ya dola bilioni 300 mwezi Septemba. 

Nyongeza hiyo ya ushuru wa asilimia 10 ambayo huenda itazilenga bidhaa za elektroniki na mavazi, itamaanisha kuwa karibu bidhaa zote za China zinapelekwa Marekani zitalipiwa kodi.

 Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni wa China, Hua Chunying, amesema pindi Marekani itaendelea na mipango yake ya kuongeza ushuru, China itajibu kwa kuchukua hatua sawa kulinda maslahi yake. 

Ingawa Chunying hakueleza hatua ambazo nchi hiyo itachukua, afisa huyo amesisitiza kuwa China haitokubali shinikizo, vitisho na ulaghai kutoka Marekani. 

Rais Trump ametishia mara kadhaa kuendelea kuongeza ushuru kwa bidhaa za China ikiwa rais Xi Jinping hatoharakisha mipango ya kufikia makubaliano ya kibiashara