NEWS

3 Agosti 2019

Huwezi Amini..KUMBE Jux Aliachwa Solemba na Vanessa Mdee...Akaamua Kulipiza Kwa Mchina

Baada ya sintofahamu ya muda mrefu kuwa ni nani alivunja penzi la Jux na Vanessa hatimae Jux amefunguka na kukubali kuachwa na mpaka leo hajajua sababu ya Vanessa kuvunja penzi lao.

Kwenye moja ya interview yake hivi karibuni Jux amesema “Kwenye mahusiano kuna wakati mapenzi yanaisha na kubaki mazoea hivyo Vanessa yeye ndiyo aliniambia kuwa anaona mahusiano yetu hayaeleweki hivyo akaomba tuachane, kiukweli iliniumiza sana na hata nilivyomuuliza sababu alinipa sababu ambazo siwezi kuziweka hadharani ila ni sababu ambazo unatakiwa uzielewe na kweli nilimuelewa"

Kwa upande mwingne Jux amefafanua sekeke la Venessa kuwa unfollow watu wake wakaribu kwa kusema

"Sijui kwanini ameamua ku- unfollow watu wangu wa karibu wote na sidhani kama ni sawa kwani kama ingekuwa kila mtu ambaye unaachana naye una- unfollow watu zake wa karibu ingekuwa mbaya zaidi, akumbuke pia hata yeye wakati naanza naye watu wangu wa karibu walimpokea vizuri licha ya mtu ambaye nilikuwa naye kwenye mahusiano kipindi kile kupata matatizo”