VIJANA kumi na tano alfu kutoka Tanganyika, walikamatwa kwa nguvu kwenda kupigana vita ya pili ya dunia ili kuikomboa uingereza dhidi ya Adolf Hitler, vijana wakampoteza Hitler, waingereza wakapiga vigelegele, vijana wa kazi wakarudi nyumbani na majina ya kishujaa kufa maskini, sasa ni wazee, hawana nguvu tena, hawaoni vizuri,hawasikii vizuri, hawana kumbukumbu nzuri, hawana meno, wengi wamekufa na huzuni moyoni, hasira kichwani, ukata mifukoni, wamebaki 400 kati ya 13,000 waliorudi, mwenye umri mdogo ana miaka 92, wengi hatujui walipo kwa sababu hatuijui historia yetu, uingereza haijui walipo kwa sababu shukurani ya punda ni mateke.
Wakati wanasagwa kwenda vitani aliyejifanya kukaidi alitupwa jela miezi sita na viboko juu, alivyotoka jela aliulizwa kuchagua kwenda vitani au kurudi jela tena miezi sita, wote walichagua kwenda vitani kupigana vita ambavyo havikuwahusu.
Tatizo la wazungu bwana, wao wakizinguana wanasema ni vita ya dunia na kutulazimisha tukawasaidie, sisi tukizinguana wanasema ni vita vya ukabira na kuja kutuuzia silaha tuuane wao wachume kwa sababu kwenye vurugu pana ulaji.
The post VIDEO: Historia Ya WATANZANIA Waliopigana Vita Ya Dunia! appeared first on Global Publishers.