MABINGWA mara 27 wa Ligi Kuu Bara, Yanga jana wamerejea ndani ya Jiji la Dar na kupokewa na mashabiki lukuki huku Kocha Mwinyi Zahera akitamka kuwa wapinzani wao wamekwisha.
Yanga ilikuwa kambini mjini Morogoro tangu Julai 7, mwaka huu na jana ilifanya mazoezi yake ya mwisho mjini humo asubuhi kisha wakarejea jijini Dar mida ya jioni.
Wakiwa njiani, walipokelewa na mashabiki lukuki ambao walikuwa wakitaka kuwaona wachezaji wao wapya ambao kesho Jumapili watatambulishwa na kucheza mechi ya kirafiki na Kariobang Shark’s ya nchini Kenya kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Baadhi ya wachezaji wapya waliosajiliwa Yanga ni kipa Mkenya, Farouk Shikalo, beki Lamine Moro (Ghana), Mustapha Suleiman (Burundi), Patrick Sibomana (Rwanda), Juma Balinya (Uganda), Issa Bigirimana (Rwanda), Sadney Urikhob (Namibia) na Maybin Kalengo (Zambia).
Pia kuna wazawa kama kipa Metacha Mnata, Muharami Issa ‘Marcelo’, Ally Ally ‘Mwarabu’, Ally Mtoni ‘Sonso’ na Abdulaziz Makame.
The post VIDEO: YANGA YATUA DAR KIBABE, YAPOKELEWA KWA SHANGWE appeared first on Global Publishers.