NEWS

4 Agosti 2019

Katibu Mkuu CCM Ammwagia Sifa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)  Dk Bashiru Ally amesema mkuu wa Mkoa wa Mwanza,  John Mongella hataondolewa  mkoani humo hadi wakamilishe kazi ya kuufanya kuwa Mkoa ambao wananchi wake watajitokeza kwa wingi kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Ametoa kauli hiyo jana Jumamosi Agosti 3, 2019 mkoani Mwanza wakati akizungumza na seneti ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini.

“Nichukue fursa hii kumpongeza Mongella anafanya kazi nzuri na ni moja ya viongozi wanaochapa kazi, mfano halisi ni pale ilipotokea ajali ya Mv Nyerere (iliyozama), alionyesha dhahiri utendaji wake, " alisema Bashiru.

Alisema maneno yanayozungumzwa kuwa mkuu huyo wa Mkoa atagombea ubunge Wilaya ya Ilemela si ya kweli, amemhakikishia kufanya naye kazi pamoja.

"Waliokuwa wanamsingizia kuwa ataenda kugombea ubunge haendi huko na akiwa king'ang'anizi atakosa vyote ubunge na ukuu wa Mkoa," alisema Bashiru.