NEWS

1 Agosti 2019

Mabao Yampagawisha Balinya Yanga

Juma Balinya.

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mganda Juma Balinya amefunguka kuwa anafurahishwa na kasi yake ya kupachika mabao ambayo amekuwa nayo katika mechi za kirafiki. Hadi sasa Balinya anashika nafasi ya pili kati ya washambuliaji ambao wamefunga mabao mengi katika mechi za kirafiki za Yanga tangu walipoweka kambi mkoani Morogoro.

 

Balinya katika mechi tano ambazo wamecheza Yanga amefunga mabao manne wakati mshambuliaji Patrick Sibomana ndiye anaongoza kwa mabao mengi akiwa nayo matano.

 

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Polisi ya Uganda amesema: “Mechi mbili zilizopita zote nimefanikiwa kufunga, hilo ni jambo zuri kwangu kwa sababu inaonyesha tunavyoshirikiana na wenzangu.

 

Huu ni mwanzo bado tunatakiwa kufanya kazi kubwa hapa Yanga.” Yanga jana Jumanne ilicheza na Friends Rangers na kushinda 2-0.

The post Mabao Yampagawisha Balinya Yanga appeared first on Global Publishers.