KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kikosi kilichoanza kwenye mchezo wa jana Jumanne ndiyo kikosi chake cha msimu huu.
Kwa mara ya kwanza kwenye maandalizi ya msimu huu, Zahera jana alipanga kikosi wakati timu yake ilipokuwa ikicheza na Friends Rangers na kupata ushindi wa mabao 2-0. Zahera ambaye alichelewa kujiunga na timu hiyo, alipanga kikosi cha jana ambacho kilionekana kuwa na mabadiliko makubwa huku akisema kuwa ameridhishwa na kila kitu.
Kikosi kilichoanza jana ni: kipa Klaus Kindoki mabeki, Ally Ally, Ally Mtoni ‘Sonso’, Mustafa Seleman, Lamine Moro, viungo, Papy Tshishimbi, Balama Mapinduzi, Raphael Daud washambuliaji, Sadney Urikhob, Juma Balinya, Patrick Sibomana.
Zahera amelieleza Championi Jumatano kuwa hana shaka na wachezaji wake kwa sasa na anaona kuwa wanaweza kufanya kile ambacho anakitaka msimu ujao.
“Kesho (leo) na keshokutwa sitakuwa na mazoezi, nataka wachezaji wangu wapumzike kwa kuwa nimeridhika kwa kile ambacho wamekifanya hapa Morogoro hadi sasa. “Hiki ulichokiona leo ndiyo kikosi changu cha kwanza kwa ajili ya msimu ujao, ukiniuliza kikosi chako cha kwanza kina nani na nani basi ni hawa walioanza leo.
“Na nimewatazama nimeona kuwa wote wapo vizuri, Ally Ally na Sadney Urikhob ndiyo nimeona bado hawapo fi ti sana lakini naamini hadi tuanze ligi watakuwa tayari. “Najua watu wanaweza kuuliza kwa nini nimemtumia Sonso kama beki wa pembeni, ndiyo nilimsajili kwa kuwa nilijua kuwa anaweza kucheza pembeni na kati.
“Huku pembeni leo amefanya kazi nzuri sana na umeona jinsi ambavyo amekuwa akifanya kazi nzuri uwanjani,” alisema Zahera. Kuhusu ishu ya Kelvin Yondani kutotua kambini Yanga, Zahera alisema kuwa alimpa mchezaji huyo mapumziko ya siku 19 na wakati anaitwa kwenye timu ya taifa kwa mara ya pili zilikuwa hazijaisha.
“Yondani atakuja, nilimpa siku 19 apumzike na hadi anaitwa tena Stars zilikuwa hazijaisha, kama ana nafasi au la, tuache kwanza nafi kiri hadi akijiunga na kambi.”
Hata hivyo, Zahera, amesema leo alfajiri atashusha mshambuliaji mwingine wa kuongezea nguvu. Mshambuliaji huyo alitarajiwa kutua usiku wa kuamkia leo saa 9 usiku. “Kesho (leo) alfajiri atashuka mshambuliaji mwingine kutoka Congo, huyo ni mtu haswa, siwezi kutaja jina wala timu yake kwa sasa nafi kiri tusubiri kwa kuwa atafi kia Dar na kutusubiri hukohuko.”
The post HUKU LIGI IKIKARIBIA… FIRST ELEVEN YANGA HII HAPA appeared first on Global Publishers.