NEWS

2 Agosti 2019

Mama Diamond: Kuna picha za ‘nguo za kuogelea’ zinakuja!


Mama Mzazi wa msanii nyota wa Bongo Fleva Diamond Platnumz Sanura Kasimu almaarufu Bi Sandra amesema suala la yeye kupiga picha na mumewe na kuziposti ni uamuzi wao na hakuna wa kuwazuia na kusisitiza kuwa zipo nyingine walizopiga wakati wakioga kwenye bwawa la kuogelea (swimming pool) lililopo nyumbani kwao na ikifika muda wataziachia mtandaoni.

Bi Sandra ameongeza kuwa ametumia gharama kubwa sana kujenga swimming pool na hivyo ni haki na wajibu wao kuitumia kwani hajatengeneza sehemu hiyo kwa sababu ya kuoga chura na kusisitiza kuwa kuna takribani picha mia tano ambazo wamepiga sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi ikiwemo Dubai.


Mama Daimon ‘Bi Sandra’ akiwa na mumewe Uncle Shamte wakati akisherehekea siku yake ya kuzaliwa. Picha kwa hisani ya ukurasa wa Instagram wa Mama Diamond.
Mimi na mume wangu lazima tupige picha tunavyojisikia, sio hizo tu zipo nyingine hatujazitoa mpaka nyingine tumepiga kwenye swimming pool tunaoga zipo. Swimming pool maana yake kuoga, kama umeweka swimming pool halafu huogielei unataka waoge vyura? Nyingine tumepiga dubai, nimejenga swimming pool kwa bei halafu aoge nani? Ndiyo kuna picha nipo mimi na mume wangu tunaogelea,” amesisitiza Bi Sandra akiwa pembeni ya mumewe.

Amesema picha hizo wataziachia kwa awamu na hawamuhofii mtu yeyote huku mumewe maarufu kwa jina la Uncle Shamte akisisitiza kwa kusema kuwa swimming pool ina mavazi yake na imetengenezwa kwaajili ya kuogelea na sio kuangalia na kuongeza kuwa huwa wanaogelea kila siku.


Ukiona picha tunaoga basi ni kitu cha kawaida, kinachotusumbua sisi (siwezi kusema ulimbukeni au ushamba) bali ni kutokujua tu. Mtu mwingine anajua labda swimming pool kazi yake ni kuchukua vyura na kuwarusha mle ndani, lakini ipo ndani ya compound (eneo), ipo nyumbani, kwa maana tunaooga ni sisi ambao tunakaa pale, amesema Uncle Shamte huku Bi Sandra naye akidakia na kusema: Tumejenga kwa bei kubwa, bei ya gharama, sasa tuiache tu waogelee vyura, wapige makelele. Tunaoga wenyewe, tunapiga picha.

Amesisitiza kuwa lengo la kupiga picha sio kuwanyoosha watu ila wanafanya hivyo pale wanapojisikia.