NEWS

4 Agosti 2019

Pogba aanza kufanya vitimbi, Agomea Safari

PAUL Pogba amechukua hatua ya kulazimisha kuondoka Manchester United baada ya kugoma kusafiri na timu hiyo kwenda Wales kwa ajili ya mechi ya kirafiki. Staa huyo hakutokea uwanja wa ndege wa Manchester juzi kwa ajili ya kusafiri na timu iliyokuwa inakwenda Cardiff kwa mchezo wa kujipima nguvu.

Manchester United ilicheza na AC Milan jana mjini Cardiff ikiwa ni mechi ya kujiandaa na msimu mpya wa 2019/20.

 

Gazeti la Daily Mail la Uingereza limepata taarifa za kuaminika kuwa Pogba aligomea safari hiyo ili kushinikiza suala lake la kuondoka katika klabu hiyo. Hata hivyo, klabu ya Manchester United ilitoa taarifa ikidai kuwa Pogba hakusafari kwa kuwa alikuwa na tatizo la mgongo.

Ndege iliyowabeba Manchester United ilichelewa kuondoka kutokana na kumsubiri Pogba, ambaye hakutokea.

 

Hata hivyo, habari zaidi zinaeleza kuwa Pogba alishapanga kutokwenda Wales na aliwaambia wenzake mapema.

 

Wakala wake Mino Raiola yupo England ingawa kwa shughuli ya kukamilisha uhamisho wa straika wa Juventus, Moise Kean kujiunga na Everton.

 

Hata hivyo, habari zinaeleza kuwa Raiola pia anashughulikia suala la Pogba kujiunga na Real Madrid ambako amekuwa anatakiwa kwa muda mrefu sasa. Manchester United, hata hivyo, imeweka msimamo wake wazi kuwa haina mpango wa kumuuza Pogba.

The post Pogba aanza kufanya vitimbi, Agomea Safari appeared first on Global Publishers.