TAIFA Stars ambayo itakuwa ikitazamwa na Rais John Pombe Magufuli leo kupitia runinga, inahitaji sare ya mabao au ushindi jioni hii dhidi ya Kenya ili kusonga mbele kwenye harakati za kufuzu CHAN.
Katika mechi ya awali timu hizo zilitoka suluhu Jijini Dar es Salaam katika mchezo ambao Stars ilitawala kwa kila kitu. Kenya inaingia uwanjani ikiwa na morali ya chini kutokana na wachezaji kutolipwa posho zao huku viongozi wao wakizozana na serikali kutokana na malipo hayo.
Wiki hii ilitishia kujitoa kwenye mchezo huo kutokana na ishu hiyo ya fedha, huku kocha akiwasisitiza mashabiki wajitokeze leo kufufua morali ya wachezaji.
Kaimu Kocha Mkuu wa Stars, Mrundi, Etienne Ndayiragije ameliambia Spoti Xtra kuwa, wamejiandaa vya kutosha kwa ajili ya mchezo huo na anaamini kabisa wataitupa Kenya nje ya michuano hiyo.
“Kila kitu kuhusiana na mchezo kipo sawa na tumejipanga vilivyo ili kuhakikisha tunaibuka na ushindi,”alisema kocha huyo wa zamani wa KMC.
“Wachezaji wote tuliokuja nao huku wapo vizuri, nimatumaini yangu kuwa wataipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika mchezo huo,” alisema Ndayiragije ambaye timu yake ya Azam inashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho msimu huu
The post Stars kanyaga twende dhidi ya Kenya leo appeared first on Global Publishers.