DAR ES SALAAM: Saa chache baada ya mwanamama wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ kudai kuwa Rais wa Wasafi, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anabagua wasanii katika tamasha lao la Wasafi, makamu wa rais wa lebo hiyo, DJ Romy Jones amemjibu. Matukio hayo yote yalijiri juzi kwenye hafla ya kusikiliza Albam ya Changes ya DJ Romy Jones iliyofanyika kwenye Viwanja vya Samaki-Samaki ndani ya Mlimani City jijini Dar. Katika ishu hiyo Shilole alifunguka; “Nataka nione Wasafi Festival wakichukua wasanii kama walivyokuwa wanafanya watu wengine.
“Wasafi Festival tumezoea kumwona Rayvanny, Lava Lava, Harmonize na Diamond. Diamond ajaribu kuongeza wasanii wengine kwa sababu amesema hii ni yetu sote, kweli iwe yetu sote, siyo yetu sote kwenye mitandao, lakini ndani hakuna cha yetu sote. “Naongea kutoka moyoni kwa sababu wasanii wengine wanaleta malalamiko kwangu. “Mimi ninamwambia kama kaka yangu, hii yetu sote, iwe yetu sote kweli!
“Ziara zake (Diamond) anazokwenda achukue na wasanii wengine na siyo Wasafi pekee. “Kuna wasanii wengi, aongeze. Kuna Roma, Stamina na Maua Sama. Hata mimi asiponichukua, sijali.” Kwa upande wake, DJ Romy Jones alimjibu; “Kipindi cha kwanza tulipomchukua Young Killer, tulimwacha Bilnas.
“Watu wakaanza kusema, lakini ukweli ni kwamba muda wa Bilnas ulikuwa haujafika. Sasa hivi tumemchukua Bilnas, labda tumemwacha tuseme Dudu Baya. “Dudu Baya muda wake ulikuwa umeisha so kila kitu kina muda wake, kila mtu ana muda wake. Kila mtu ataonekana kwa muda wake.”
The post Romy Jones amjibu Shilole! appeared first on Global Publishers.