KOCHA wa Simba Patrick Aussems tayari amekabidhiwa video za wapinzani wao UD Songo ya kutoka Msumbiji. Simba itavaana na UD Songo Agosti 10, mwaka huu huko jijini Beira ukiwa ni mchezo wa mtoano wa Ligi ya Mabingwa Afrika na watarudiana Agosti 25, mwaka huu jijini Dar.
Kwa sasa vijana hao wa Msimbazi wapo kwenye maandalizi ya tamasha lao la Simba Day litakalofanyika Uwanja wa Taifa Jumanne ijayo kwa kucheza na Power Dynamos ya Zambia.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Mbelgiji alisema kuwa, baada ya kupatiwa video hiyo tayari ameanza kuwasoma wapinzani wake hao kwa kuangalia mbinu mbalimbali ambazo wanazitumia wakiwa ndani ya uwanja.
“Tayari nimekabidhiwa video za wapinzani wetu UD na nimeanza kuzifanyia kazi kwa ajili ya kuwa soma vizuri na kujua ni mbinu gani ambazo wanatumia ili kuona ni namna gani tunapata ushindi ugenini,” alisema Aussems. Aidha, Katibu wa Simba, Dk Anorld Kashembe alisema kuwa, tayari Simba ilishatuma mashushu kwa ajili ya maandalizi kuelekea mchezo huo.
“Mchezo utapigwa Agosti 10, mwaka huu pale Beira na Simba itaondoka hapa Bongo Agosti 9, mwaka huu kwenda huko kwa ajili ya mchezo huo muhimu.
“Kuna watu tayari wametangulia kwenda kusoma mazingira na kujua timu inafika wapi na wapinzani wetu wanafanya nini lakini taarifa zaidi zitatolewa kwenye mkutano ambao utafanyika hivi karibuni,” alisema Kashembe.
SHANGWE La YANGA Walivyofika HOTELINI Magomeni, MAKAMBO Atajwa!
The post Simba SC yanasa video ya wapinzani wao Caf appeared first on Global Publishers.