NEWS

1 Agosti 2019

Tundu Lissu "Mimi na Timu Yangu Tutatinga Mahakamani Kuu Wakati Wowote Tupo Tayari"


Aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, amesema yeye na timu yake wako tayari kutinga Mahakama Kuu muda wowote  kuanzia leo maandalizi yote yanayohitajika yamekamilika.

Lissu aliyasema hayo kupitia akunti yake ya Twitter kuwa kesi za ubunge ni kesi za kisiasa. Ni kesi nyeti na zinahitajika umakini mkubwa katika kuziandaa na kuziendesha.

“Mimi na timu ya mawakili wangu tupo tayari kuingia Mahakama Kuu ya Tanzania. Tutafanya hivyo muda wowote kuanzia leo maandalizi yote yanayohitajika yamekamilika,” aliandika Lissu.

Lissu alieleza kuwa atawajulisha mara moja kesi hiyo itakaposajiliwa rasmi.

“Kama itawapendeza nitawaomba mtakaopata nafasi kuhudhuria mahakamani kwa niaba yangu wakati wowote kesi hiyo itakapokuwa inaendelea,” alieleza Lissu.

 Kesi za ubunge ni kesi za kisiasa. Ni kesi nyeti na zinahitaji umakini mkubwa katika kuziandaa na kuziendesha.

Mimi na timu ya mawakili wangu tuko tayari kuingia Mahakama Kuu ya Tanzania. Tutafanya hivyo muda wowote kuanzia leo. Maandalizi yote yanayohitajika yamekamilika.


Tundu Antiphas Lissu
@TunduALissu
Nitawajulisheni mara moja kesi hii itakaposajiliwa rasmi. Kama itawapendeza, nitawaomba mtakaopata nafasi kuhudhuria mahakamani, kwa niaba yangu, wakati wote kesi hiyo itakapokuwa inaendelea.

21
5:26 PM - Jul 31, 2019
Twitter Ads info and privacy
See Tundu Antiphas Lissu's other Tweets
AMEHITIMISHA KUTUMIA DAWA

Aidha, Lissu ameeleza kuhitimisha matumizi ya dawa alizoanza kutumia tangu Septemba 7 mwaka 2017 na sasa yupo tayari kurudi Tanzania September 7 mwaka huu.