KWELI hii kali! Mrembo kutoka Bongo Flevani, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amefichua siri kwa kusema katika maisha yake haongeagi na wanaume pasua kichwa mara mbili zaidi ya kuwachapa makofi.
Lulu amesema mwanaume yeyote aliyewahi kutoka naye kimapenzi anajua vibao vyake maana anasema ana mkono mwepesi mwanaume akimletea za kuleta.
“Yaani nikiona kama mwanaume ananizingua anachezea vibao fasta, vibao vyangu siyo mchezo wananijua wote waliowahi kukutana navyo hususan waliowahi kuwa na mimi,” alisema Lulu.
Baadhi ya wanaume waliowahi kuwa na mahusiano na Lulu Diva ni pamoja na jamaa anayejulikana kwa jina moja la Joh na staa wa Bongo Fleva, Rich Mavoko.