NEWS

31 Desemba 2019

Upelelezi Kesi ya aliyemchoma moto mke wake wakamilika

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa upelelezi wa kesi inayomkabili Mfanyabiashara Khamisi Luwonga anaedaiwa kumuua Mkewe Naomi Marijani kwa kumchoma kwa kutumia gunia mbili za mkaa umekamilika.

Wakili wa Serikali Mwandamizi Simon Wankyo ameyasema hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Salum Ally, wakati kesi hiyo ilipofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa, ambapo imepigwa kalenda hadi siku ya Januari 7, 2020, itakapotajwa tena.

Mfanyabishara huyo, anadaiwa kutenda kosa hilo Mei 15, 2019, nyumbani kwake maeneo ya Gezaulole Kigamboni, baada ya kumuua na kisha kumchoma moto wa magunia mawili ya mkaa mke wake na kisha kuyabeba mabaki ya mwili huo na kwenda kuyafukia shambani kwake Mkuranga.