NEWS

30 Januari 2020

Bunge la Ulaya lapiga kura kuruhusu Uingereza kuondoka EU

Wabunge wa bunge la Umoja wa Ulaya wamepitisha kwa wingi sheria inayoruhusu Uingereza kuondoka kwenye Umoja huo ama Brexit, wiki hii na kuondoa kizingiti kikubwa cha mwisho kabla Brexit yenyewe kufanyika. 

Bunge hilo limepiga kura ya kuyapitisha makubaliano ya Brexit kwa kura 621 dhidi ya 49 ambao walipinga. 

Kulitakiwa wingi mdogo wa kura kwenye bunge hilo lenye wabunge 75. 

Nchi wanachama hivi sasa wanatakiwa kutoa idhini ya mwisho kwenye makubaliano hayo kupitia utaratibu wa maandishi. 

Uingereza inataraji kuondoka Umoja wa Ulaya usiku wa kuamkia Ijumaa, baada ya miaka mitatu tangu Waingereza walipoanzisha mchakato wa kuondoka ama kusalia kwenye Umoja huo, katika kura ya maoni ya mwaka 2016.