NEWS

29 Aprili 2020

Korea Kaskazini “Kim Jong Un yuko fiti” Sio Mara ya Kwanza Kwenda Mafichoni


Rais Donald Trump wa Marekani amesema kwamba anajua hali ya Kim Joing un , kufuatia madai kuhusu afya ya kiongozi huyo wa Korea Kaskzini.

Rais huyo alisema kwamba hawezi kutoa maelezo lakini anatumai kwamba bwana Kim yuko shwari.

Kumekuwa na uvumi uliokuwa ukizunguka tangu bwana Kim alipokosa kuhudhuria sherehe za kuadhimisha siku kuu muhimu.

Hatahivyo Maafisa wa Korea Kusini wanasema kwamba hakuna lisilo la kawaida nchini Korea Kaskazini.

Katika kikao cha faragha siku ya Jumapili waziri anayehusika na maswala ya kuleta amani kati ya mataifa hayo mawili Kim Yeon – chul alisema kwamba serikali ina uwezo wa kiintelijensia kusema kwamba hakuna kisicho cha kawaida kilichokuwa kikifanyika nchini humo.

Uvumi kuhusu hali ya kiafya ya kiongozi huyo wa Korea Kaskazini ulianza baada ya kutoonekana katika maadhimisho ya sikukuu ilofanyika tarehe 15 mwezi Aprili.

Vyombo vya habari vya Korea Kusini wiki iliopita viliripoti kwamba Kim Joing un huenda alifanyiwa upasuaji wa moyo ama alikuwa amejitenga ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Hatahivyo pia vilisema kwamba ametuma ujumbe wa pongezi kwa wafanyakazi waliokuwa wakijenga hoteli ya kitalii katika mji wa Wonsan , eneo ambalo vyombo vya habari vya Korea Kusini vinasema huenda ndiko Kim anakoishi.

‘Msimamo wa serikali yetu ni thabiti”, Moon Chung-in, mshauri mkuu wa maswala ya kigeni wa rais wa Korea Kusini Moon Jae-in akijibu maoni ya vyombo vya habari nchini Marekani.

”Kim Jong un yuko hai na hali yake ni shwari. Amekuwa akiishi katika eneo la Wonsan tangu tarehe 13 mwerzi Aprili. Hakuna kisicho cha kawaida ambacho kimegunduliwa”, alisema akinukuliwa na chombo cha habari cha Aljazeera.

Je uvumi huo ulianza lini
Baada ya kukosa kuhudhuria sherehe ambayo hajawahi kukosa kuhusu kuadhimisha kuzaliwa kwa babu yake mnamo tarahe 15 mwezi Aprili .

Kukosekana kwake ndiko kulizua majadala wa hali yake ya afya kwa kuwa hajawahi kukosa sherehe kama hiyo .

Mara ya mwisho alionekana katika chombo cha habari cha serikali mnamo tarehe 12 mwezi Aprili akikagua kundi la ndege za kivita .

Uvumi ulianza wakati Kim Jong un alipokosa sherehe ya kuzaliwa kwa babu yakeHaki miliki ya pichaEPA
Image captionUvumi ulianza wakati Kim Jong un alipokosa sherehe ya kuzaliwa kwa babu yake
Katika ukaguzi huo alionekana kuwa mtu ambaye afya yake ilikuwa shwari.

Treni ya kibinafsi
Picha za setlaiti za wiki iliopita , zilionyesha treni maalum inayomilikiwa na Kim Jong un katika eneo la Wonsan na hivyobasi kuziongezea uzito ripoti hizo.

Wiki iliopita China ilidaiwa kutuma kundi moja la maafisa wake kwenda Korea Kaskazini wakiwemo wataalam wa kimatibabu.

Sio mara ya kwanza Kim kwenda mafichoni
Mwaka 2014, Kim Jong un alitoweka kwa siku 40 kuanzia mapema mwezi Septemba hatua iliozua uvumi mwingi , ikiwemo ule kwamba huenda amependuliwa na wanasiasa wengine.

Gazeti la Korea Kaskazini Rodong Sinmun lilichapisha picha kadhaa za kiongozi huyo akiwa amebeba mkwaju Oktoba 2014.Haki miliki ya pichaAFP
Baadaye akajitokeza akipigwa picha na mkwaju.

Vyombo vya habari vya serikali vilikiri kwamba alikua akiugua, lakini havikuzungumzia alikuwa akiugua nini.

Ripoti ya kuugua
Madai kwamba afya ya Kim Jong Un ilikuwa mbaya yalijitokeza katika ripoti ya tovuti iliokuwa ikimilikiwa na watoro wa Korea kaskazini.

Mara ya mwisho Kim Jong un alipigwa picha katika sherehe ya kukagua gwaride tarehe 12 ApriliHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMara ya mwisho Kim Jong un alipigwa picha katika sherehe ya kukagua gwaride tarehe 12 Aprili
Chanzo ambacho hakijulikani kiliambia gazeti la kila siku la DK kwamba wanaelewa amekuwa akiugua ugonjwa wa moyo tangu mwezi Agosti , lakini hali hiyo ikazidi kuwa mbaya baada ya kuzuru mlima Paetku mara kwa mara.

Hatua hiyo ilivifanya vyombo vya habari vya kimataifa kuanza mjadala