NEWS

30 Aprili 2020

Lilian, Mtanzania Aliyefungwa Miaka 18 Indonesia… Kampigia Simu Millard Ayo Toka Gerezani


Aliondoka Tanzania kwa kushawishiwa na Rafiki mwenye pesa, nyumba na gari za kifahari, Rafiki alimwambia Malaysia kazi za maana zipo njenje lakini alichokikuta Malaysia ni tofauti na alichoambiwa, Rafiki huyo akamgeuzia kibao na kumwambia kazi pekee ni ya dawa za kulevya, kwa shingo upande Lilian akakubali kubeba dawa za kulevya kwa mara ya kwanza maishani mwake kwa kuzisafirisha kutoka Malaysia hadi Indonesia.

Kwenye hiyohiyo safari yake ya kwanza akakamatwa baada tu ya kutua Airport Malaysia, Polisi wakaweka mtego ili wawanase waliokua wanasubiri kuupokea mzigo, kwa siku 3 Lilian aliwekwa chini ya ulinzi Hotelini Polisi wakiwasubiria Wapokeaji wa hizo dawa….. siku ya tukio wakaweka mtego na kumbeba Lilian kwenye gari lao, nini kilifata?

Lilian ambae sasa hivi tunavyoongea yupo gerezani Indonesia akitumikia kifungo cha miaka 18 anatumia simu aliyouziwa kimagendo gerezani kuongea na Millard Ayo na kusimulia yote ambapo hii hapa chini ni sehemu ya kwanza ya simulizi yake…