NEWS

29 Aprili 2020

Lyyn wa Mondi Ashinda Ofisini Kwa Kiba


HIVI karibuni zimesambaa tetesi mitandaoni kuwa msanii chipukizi wa Bongo Fleva, Irene Louis ‘Lyyn’ ameshinda ofisini kwa staa wa muziki huo, Ali Salehe Kiba ‘King Kiba’ kwa ajili ya kuomba kolabo na jamaa huyo.

Inafahamika kwamba, Lyyn ni zilipendwa wa staa mwingine wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye ni hasimu wa Kiba, hivyo tetesi hizo zilikuwa za moto ile mbaya.

Haikuishia hapo, kwani baadhi ya watu walidai kwamba, mrembo huyo aliamua kufanya hivyo baada ya kuona mwanamitindo na msanii mwenzake wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto kushiriki kwenye Wimbo wa Dodo wa Kiba na kumfanya kuwa juu kistaa.

“Unaambiwa bidada Lyyn kaona wivu mwenzake (Mobeto) kuwa video queen kwenye Wimbo wa Dodo wa Kiba, sasa na yeye kaamua kumfuata Kiba ofisini kwake ili afanye naye kolabo, lakini jamaa amemtolea nje.
“Kiba kasema hawezi kufanya kolabo na….(tusi) wa mjini,” aliandika mwananzengo mmoja kwenye ukurasa wa udaku wa Instagram.
LYYN AFUNGUKA

Hata hivyo, baada ya kuona mambo yamekuwa mengi huku kila mtu akisema lake, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA lilimtafuta mwanadada huyo ambapo alikiri kwenda ofisini kwa jamaa huyo.

Lyyn alifunguka kuwa, ni kweli anatamani kufanya kolabo na Kiba, lakini si kweli kwamba amekataliwa.

“Sijakataliwa. Ni kweli nilikwenda pale ofisini kwa ishu zangu nyingine kabisa, wala siyo kwa sababu hiyo.
“Lakini mimi mwenyewe nimeshangaa kuona watu wanasema nimeenda kuomba kufanya kolabo na Ali (Kiba) halafu kanikatalia, mara sijui nini, yaani wanatunga tu.
“Nina uhakika hata Kiba mwenyewe atakuwa ameshangaa kwa sababu hatujawahi kuzungumzia ishu hiyo na wala hiyo siku hatukuonana kabisa.
“Mimi nilikwenda pale (ofisini kwa Kiba) kuonana na watu wengine, wala siyo yeye.
“Japokuwa ukweli ni kwamba, natamani sana kufanya kolabo na Ali (Kiba) kwa sababu ni mwanamuziki mkubwa, lakini binafsi sijawahi kumtafuta.
“Hata hivyo, naamini viongozi wangu siku moja watamtafuta na kuzungumza naye kuhusu ishu hiyo,” amesema Lyyn ambaye anajulikana zaidi kwa jina la Lyyn wa Mondi.

STORI: MEMORISE RICHARD, DAR