MCHORO wa mwilini (tatuu) ya sexy lady kunako Bongo Flevani, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ ni hatari tupu na imekuwa gumzo kinoma kwenye mitandao ya kijamii kutokana na sehemu aliyojichora.
Gumzo hilo lilitokana na Lulu Diva kuchora tatuu hiyo kubwa kwenye paja lake la mguu wa kulia ambapo amesema anaipenda na ana mpango wa kuchora nyingine nyuma ya paja hilo kwani ni kitu anachojivunia.
“Najua watu wameshangaa kuona ukubwa wa tatuu yangu, lakini ukweli ni kwamba naipenda mno, sijui hata nisemeje, nina mpango wa kuongeza nyingine nyuma ya paja,” amesema Lulu Diva ambaye pia ni mwigizaji wa Bongo Movies.
STORI: IMELDA MTEMA